Pata taarifa kuu
MYANMAR-MAUAJI-USALAMA

Aung San Suu Kyi alaani ukiukwaji wa haki za binadamu dhidi ya Warohingya

Kiongozi wa Myanmar, ambaye anasema «kusitikishwa mno» na mauaji yanayoendelea kuwakabili raia kutoka jamii ya Rohingya, amelihutubia taifa kutoka mji mkuu wa nchi hiyo, Naypyidaw.

Hotuba ya kiongozi wa myanmar Aung San Suu Kyi kuhusu mgogoro unaowakabiliwa raia kutoka jamii ya Rohingya katika jimbo la Arakane, Septemba 19, 2017, Naypyidaw.
Hotuba ya kiongozi wa myanmar Aung San Suu Kyi kuhusu mgogoro unaowakabiliwa raia kutoka jamii ya Rohingya katika jimbo la Arakane, Septemba 19, 2017, Naypyidaw. REUTERS/Soe Zeya Tun
Matangazo ya kibiashara

Hii ni hotuba yake ya kwanza ya kitaifa kuzungumzia ghasia zinazotokea nchini humo zilizosababisha zaidi ya watu laki nne, Waislamu kutoka jamii ya Rohingya, kukimbilia nchini Bangladesh, wiki chache zilizopita.

Ujumbe huu pia umeelekezwa kwa jumuiya ya kimataifa wakati ambapo kunafunguliwa Jumanne hii Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa. Aung San suu Kyi hatashiriki mkutano huo. Hotuba hii iliyorushwa moja kwa moja kwenye televisheni ya taifa ilikua ikisubiriwa kwa hamu na gamu.

Hata hivyo Aung San Suu Kyi ameendelea kuonyesha uungwaji wake mkono kwa jeshi ambalo linashtumiwa kuendesha mauaji dhidi ya Waislam kutoka jamii ya Rohingya kwa hoja ya kupambana dhidi ya magaidi.

Aung San Suu Kyi ambaye pia ni mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel, amekuwa akishinikizwa kimataifa kutoa tamko lake juu ya jeshi la nchi yake, ambalo linatuhumiwa kuwaua na kuwatesa watu hao.

Mataifa ya nchi za magharibi na Umoja wa Mataifa umeitaka Myanmar kumaliza dhulma hiyo na kuwaruhusu wakimbizi hao kurejea nchini mwao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.