Pata taarifa kuu
MYANMAR-MAUAJI-USALAMA

Waasi wa Rohingya wakanusha kushirikiana na makundi ya kigaidi

Wapiganaji wenye silaha wa Rohingya ambao walifanya shambulio magharibi mwa nchi ya Myanmar na kusababisha jeshi la nchi hiyo kufanya operesheni iliyosababisha janga la kibinadamu, wamekanusha kuwa na uhusiano na makundi mengine ya kigaidi duniani.

Watu kutoka jamii ya Rohingyawaendelea kukimbili katika nchi ya, Bangladesh,Septemba 10, 2017.
Watu kutoka jamii ya Rohingyawaendelea kukimbili katika nchi ya, Bangladesh,Septemba 10, 2017. REUTERS/Danish Siddiqui
Matangazo ya kibiashara

Kauli hii wanayoitoa saa chache baada ya mtandao wa Al-Qaeda kuwataka waislamu kuungana kujibu mashambulizi.

Kundi hilo la The Arakan Rohingya Salvation Army limesema inachokifanya ni kulinda haki za jamii ya Rohingya wakati huu ambapo pia umoja wa Mataifa kupitia baraza la usalama na katibu mkuu Antonio Guterres wakitaka kukomeshwa kwa mauaji dhidi ya raia nchini Myanmar.

Haya yanajiri wakati huu maelfu ya raia wa Rohingya wakiendelea kuyakimbia makazi yao nchini Myanmar na kuingia kwenye nchi ya Bangladesh.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.