Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 23/06 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 23/06 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 23/06 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Asia

Jeshi la Urusi kuonyesha nguvu zake kwa Umoja wa Ulaya

media Le président Vladimir Poutine lors d'une intervention au Forum économique international de Saint-Pétersbourg, ce vendredi 2 juin 2017. REUTERS/Grigory Dukor

Urusi inatazamia kuzindua Alhamisi hii mazoezi makubwa ya kijeshi pamoja na Belarus, ambayo inasisitiza kuonyesha kama ya "kujihami" lakini yameshtumiwa na baadhi ya wanachama wa Umoja wa kujihami wa nchi za Magharibi (NATO) kama maonyesho ya nguvu.

Moscow inajaribu kutuliza nyoyo kwa mazoezi haya, yaliyopewa jina la Zapad-2017 ("West-2017") ambayo yatashirikisha takriban askari wake 12,700 kwa muda wa wiki kwenye mpaka na Lithuania na Poland.

Mkuu wa majeshi ya Urusi, Valeri Guerassimov, alihakikisha mapema mwezi Septemba wakati wa mkutano katika mji wa Baku na Mkuu wa Kamati ya Majeshi ya NATO, Czech Petr Pavel, kwamba mazoezi hayo " yalipangwa kwa muda mrefu" na "hayataendeshwa dhidi ya nchi yeyote".

Kila mwaka jeshi la Urusi linaandaa mazoezi makubwa ya kijeshi katika eneo tofauti na Urusi. Mwaka huu mazoezi haya yanafanyika Belarus, katika kambi ya Kaliningrad na katika mikoa kadhaa ya kaskazini-magharibi mwa Urusi.

Kwa maneno mengine, Poland na nchi za Baltic tangu Crimea kuunganishwa na Urusi mnamo mwaka 2014 na kuzuka kwa vita mashariki mwa Ukraine walikuwa tayari kushtumu Urusi kama tishio kwa uhuru wao.

Baadhi ya nchi, Lithuania na Estonia, wana mashaka na idadi ya askari waliotangazwa na Urusi kushiriki mazoezi hayo ya kijeshi na kudai kwamba "zaidi ya laki moja ya askari" watashiriki mazoezi hayo ya tarehe 14 hadi 20 Septemba.

Mazoezi ya Zapad-2017 "yamepangwa kutuchokoza, kuchunguza ulinzi wetu na ndiyo sababu tunapaswa kuwa na nguvu," Waziri wa Ulinzi wa Uingereza Michael Fallon alisema siku ya Jumapili.

Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg amesema hajaona "tishio lolote kwa Urusi kama mshirika", lakini amesikitishwa na kukosekana kwa uwazi.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana