Korea Kaskazini: Tutaendelea kutengeneza silaha za nyuklia
Nchi ya Korea Kaskazini hii leo imesisitiza kuwa itaendelea na mradi wake wa kutengeneza silaha za nyuklia kama majibu ya kile ilichosema ni vikwazo ilivyowekewa na baraza la usalama la umoja wa Mataifa.
Imechapishwa:
Akizungumza jijini New York Marekani balozi wa Korea Kaskazini kwenye umoja huo Han Tae Song amesema kilichofanywa na baraza la usalama hakitaacha kipite kwakuwa umoja huo umedhamiria kuiumiza nchi yake.
Kwa upande wake rais wa Marekani Donald Trump amesema vikwazo hivi licha ya kuwa havitakuwa na athari kubwa sana kwa Korea Kaskazini lakini vinatuma ujumbe kuwa dunia imechoshwa na kejeli za Pyongyang.
Vikwazo hivi vimechukuliwa baada ya juma moja lililopita utawala wa Pyongyang kufanya jaribio kubwa zaidi la silaha ya nyuklia.