Pata taarifa kuu
UNSC-KOREA KASKAZINI-USALAMA

Umoja wa Mataifa waiwekea vikwazo vipya Korea Kaskazini

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipitisha kwa kauli moja vikwazo vipya dhidi ya Korea Kaskazini siku ya Jumatatu, Septemba 11. Vikwazo hivyo ambavyo ni kama adhabu ya kufanyia majaribio zana zake za nuklia, vinalenga kuhujumu uwezo wa Pyongyang kufadhili na kutoa kawi kwa mpango wake wa nuklya.

Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa anazungumza na balozi wa China katika Umoja wa Mataifa baada ya mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu kesi ya Korea Kaskazini, Septemba 11.
Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa anazungumza na balozi wa China katika Umoja wa Mataifa baada ya mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu kesi ya Korea Kaskazini, Septemba 11. REUTERS/Stephanie Keith
Matangazo ya kibiashara

Miongoni mwa vikwazo hivyo ni pamoja na kupiga marufuku mauzo ya nguo kutoka Korea Kaskazini na kupunguza kiwango cha mafuta na gesi. Kwa masharti haya mapya, wanadiplomasia wana matumaini ya kuzuia 90% ya mauzo ya nje ya Korea Kaskazini na kupunguza mauzo yake ya mafuta kwa 30%. Vikwazo hivyo vilichukuliwa kwa pendekezo la Marekani, lakini si kama utawala wa Trump ulivyotarajia.

Vikwazo hivyo ambavyo sasa ni vya nane, vinaungwa mkono na China na Urusi, washirka wa karibu wa Korea Kaskazini, na vinalenga kuiadhibu nchi hii kwa kufanyia majaribo ya zana zake za nyuklia ya Septemba 3. Kwa vikwazo vyake vikali, Umoja wa Mataifa unataka kushinikiza Pyongyang kujadili mipango yake ya mpango wake wa nyuklia na ya kawaida, mipango ambayo inaelezwa kuwa inatishia utulivu wa kimataifa.

Kwa upande wa Marekani, Uingereza, Ufaransa au Italia, azimio lililopitishwa siku ya Jumatatu ni "vikali" na vyenye "uwiano". Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Nikki Haley, alikaribisha msimamo wa China na Urusi kwa kuunga mkono vikwazi hivyo na kutuma ujumbe wa umoja. "Leo tunasema kwamba ulimwengu hautakubali Korea Kaskazini kuendelea na zana zake za nyuklia. Na leo Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linasema kuwa kama Korea Kaskazini haitoachana na mpango wake wa nyuklia, tutachukua hatu sis wenyewe, " amesema Balozi Nikki Haley.

Nikki Haley, hata hivyo, alitaka kupunguza mivutano akibaini kwamba, tofauti na wiki iliyopita, bado kuna nafasi ya mazungumzo. "Hatutaki vita. Utawala wa Korea Kaskazini haujafikia hatua ya kukata kutekeleza matakwa ya jumuiya ya kimtaifa. Ikiwa itakubaliana kukomesha mpango wake wa nyuklia, itakua na mustakabali mzuri, " ameongeza balozi Nikki Haley.

Korea Kusini imesema kuwa kwa kuhujumu amani Korea Kaskzini itaewekewa vikwazo zaidi vya kimataifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.