Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/02 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/02 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/02 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Asia

Mikheil Saakashvili: Napaswa kuhaki yangu kama raia wa Ukraine

media Rais wa zamani wa Georgia na mpinzani mkuu wa rais wa Ukraine, Mikheil Saakashvili (katikati), akakiambatana na mwanasiasa mwengine wa upinzani Yulia Tymoshenko, aliporejea nchini, tarehe 10 Septemba 2017. REUTERS/Valentyn Ogirenko

Rais wa zamani wa Georgia Mikheil Saakashvili akiwa na wafuasi wake wameingia nchini Ukraine kwa nguvu, licha ya nchi hiyo kumpkonya uraia.

w. Saakashvili amesema ameamua kurudi nchini Ukraine ili kwenda Mahakamani, kupinga kupokonywa uraia wake kwa sababu anataka kurejea katika ulingo wa kisiasa nchini humo.

Bw. Saakashvili ambaye awali alikuwa ni raia wa Georgia na kisha raia wa Ukrain kwa sasa hana uraia wa nchi yoyote baada ya uraia wake wa Ukrain kufutwa na mshirika wake wa zamani raid Petro Poroshenko.

Mikheil Saakashvili alisema kuwa alisukumwa bila kutarajia kwenye mpaka na umati wa watu waliokuwa wamekasirika kutokana na kufungwa kwa mpaka.

Maafisa nchini Ukraine wanasema kuwa aliiangia nchini humo kinyume na sheria na walinzi 15 na mpaka walijeruhiwa.

Wachambuzi wa siasa nchini Ukraine wanasema kuwa rais huyo wa zamani wa Georgia aliyeongoza kati ya mwaka 2004 hadi 2013 anaonekana kuwa mpinzani mkubwa wa rais Petro Poroshenko.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana