Pata taarifa kuu
MYANMAR-UN

Guterres asikitishwa na oparesheni za kikatili dhidi ya raia Myanmar

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesikitishwa na operesheni katili za kiusalama zinazotekelezwa dhidi ya raia katika jimbo la Rakhine nchini Myanmar.

Katibu mkuu wa umoja wa Mataifa, Antonio Guterres
Katibu mkuu wa umoja wa Mataifa, Antonio Guterres
Matangazo ya kibiashara

Hatua hiyo inakuja wakati huu ambapo maelfu ya watu wa kabila la Rohingya wakikimbilia nchi jirani ya Bangladesh.

Kwa mujibu wa msemaji wake Guterres watu wanahitaji kujizuia ili kuepuka kutokea kwa janga la kibinadamu huku akitolea wito utulivu na kukumbusha kwamba serikali ina wajibu wa kuhakikisha usalama na msaada kwa wale wenye mahitaji.

Kando na kushukuru juhudi za mamlaka ya Bangladesh ambayo inajaribu kutimiza mahitaji ya wakimbizi Katibu Mkuu amesema wimbi la vurugu zilizoanza juma lililopita na mashambulizi ya vikundi vya waasi dhidi ya serikali vinahitaji kukabiliwa kiujumla ili kutatua mizizi inayochochea vurugu.

Zaidi ya warohingya 27,000 wengi wao wakiwa waislamu wamekimbia nchi jirani huku maelfu wakiripotiwa kukwama.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.