Pata taarifa kuu
KOREA KASKAZINI-MAREKANI

Korea Kaskazini yarusha makombora matatu ya masafa mafupi

Korea ya Kaskazini imerusha makombora matatu ya masafa mafupi leo Jumamosi, jeshi la Marekani limesema, hatua inayokuja baada ya majuma kadhaa ya mvutano ulioongezeka kati ya Washington na Pyongyang.

Viongozi wa mataifa yanayovutana Korea Kaskazini na Marekani
Viongozi wa mataifa yanayovutana Korea Kaskazini na Marekani ©SAUL LOEB, Ed JONES / AFP
Matangazo ya kibiashara

Uzinduzi wa kombora hayo unakuja wakati huu maelfu kwa maelfu ya majeshi ya Korea Kusini na Marekani yakishiriki katika mazoezi ya pamoja nchini Korea Kusini, ambapo Pyongyang inayaona mazoezi hayo kama majaribio ya uchokozi wa hali ya juu kwa ajili ya uvamizi wa eneo lake.

Msemaji wa kikosi cha Marekani cha Pacific amesema kuwa makombora mawili yalishindwa na moja limelipuka mara moja huku kukiwa hakuna kombora miongoni mwayo lenye madhara kwa Korea yenyewe au eneo la Guam .

Wachambuzi nchini Korea Kaskazini wanasema kuwa hilo ni jaribio la chini lenye azma ya uchokozi kujibu hatua za mazoezi ya pamoja ya kijeshi yanayoendelea nchini Korea Kusini kati ya Marekani na Korea Kusini.

Marekani na Korea Kusini zilianza mazoezi ya pamoja ya kijeshi mapema siku ya Jumatatu , majuma kadhaa baada ya mvutano mkali baina ya Pyongyang na Washington kiasi cha kutishiana.
 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.