Pata taarifa kuu
THAILAND-HAKI

Kibali cha kukamatwa chatolewa dhidi ya Yingluck Shinawatra

Waziri mkuu wa zamani wa Tahailand anayekabiliwa na kifungo cha miaka kumi jela, amekosekna wakati wa kusikiliza hukumu ya kesi yake Ijumaa hii nchini Thailand. Wakati huo huo kibali cha kukamatwa kimetolewa dhidi yake.

Waziri wa zamani wa Thailand Yingluck Shinawatra akizungukwa na wafuasi wake mbele ya Mahakama Kuu, Agosti 1, 2017.
Waziri wa zamani wa Thailand Yingluck Shinawatra akizungukwa na wafuasi wake mbele ya Mahakama Kuu, Agosti 1, 2017. REUTERS/Aukkarapon Niyomyat
Matangazo ya kibiashara

"Wakili wake anasema Bi. Shinawatwa ni mgonjwa na ameomba mahakama kuahirisha kikao cha kutoa hukumu. Mpaka sasa mahakama haijaamini kuwa Yingluck Shinawatra ni mgonjwa na kuamua kutoa kibali cha kukamatwa," amesema Jaji Cheep Chulamon mbele ya waandishi wa habari waliokuja kuhudhuria uamuzi huu.

Mwanzoni, hakuna taarifa iliyotolewa kuhusu sehemu alipo Yingluck Shinawatra, mwenye umri wa miaka 50 na mama mtoto mmoja.

Wakati wote alisema kuwa hatokimbia nchi yake kama alivyofanya ndugu yake Thaksin, aliyekuwa waziri mkuu pia, ambaye alikimbilia uhamisho mwaka 2008 baada ya kifungo cha miaka miwili gerezani kwa kashfa ya ufisadi . Kesi ambayo pia alikanusha wakati huo akisema ilikua ya kisiasa.

Maelfu ya wafuasi wake na askari zaidi ya 4,000 wa vikosi vya usalama walikuepo nje ya Mahakama Kuu. Hali ambayo ilionekana tata Ijumaa asubuhi.

Wakati huo huo Mahakama ya Juu nchini Thailand imeahirisha kikao cha kutoa hukumu katika kesi ambapo waziri mkuu wa zamani wa nchi hiyo Yingluck Shinawatra ameshtakiwa makosa ya uhalifu ya kuzembea kazini.

Bi Yingluck, ambaye alikuwa waziri mkuu wa kwanza mwanamke nchini Thailand mwaka 2011, aliondolewa madarakani mwaka 2015.

Kesi dhidi yake iliwasilishwa na serikali inayoungwa mkono na jeshi ambayo ilimuondoa mamlakani.

Lakini bado ni maarufu na anaungwa mkono sana.

Mamia ya wafuasi wake walikusanyika nje ya Mahakama ya Juu mjini Bangkok kabla ya kusomwa kwa hukumu dhidi yake, huku polisi wengi wakishika doria nje ya mahakama hiyo.

Mpango wa Bi Yingluck wa kulipia sehemu ya gharama ya mpunga ulikuwa sehemu ya ahadi zake kuu kwenye kampeni yake ya kutaka kuchaguliwa, na aliuzindua mwaka 2011 muda mfupi baada yake kuingia madarakani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.