Pata taarifa kuu
Iran-URANIUM-USHIRIKIANO

Iran yatishia kuzalisha uranium kwa kiwango kikubwa

Iran inaweza kuendelea na na mpango wa kuzalisha uranium yenye nguvu ikiwa Marekani itajitoa kwenye mkataba wa nyuklia, mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki nchini Iran (OIEA) ameonya Jumanne hii Agosti 22.

Picha ya satelaiti ya kituo cha pili cha uboreshaji wa uranium karibu na jiji la Qom, tarehe 25 Septemba 2009.
Picha ya satelaiti ya kituo cha pili cha uboreshaji wa uranium karibu na jiji la Qom, tarehe 25 Septemba 2009. (Photo : Reuters)
Matangazo ya kibiashara

"Ikiwa tutachukua uamuzi, tutaweza kuwa tumeanza ndani ya siku tano uboreshaji wa 20% (katika kituo cha nyuklia cha Fordo)," Ali Akbar Salehi ameiambia televisheni ya Irib, akisema Iran haitaki yote hayo yatokee.

Siku ya Jumanne juma lililopita rais Rohani alitishia kujitoa "ndani ya muda mfupi sana" kabla ya siku chache kwenye makubaliano ya nyuklia na nchi zenye nguvu kama Marekani itaendelea na sera yake ya "vikwazo na kulazimisha".

Makubaliano ya nyuklia ambayo yalifikiwa mnamo mwezi Julai 2015 kati ya Iran na nchi zenye nguvu duniani, yaeleza wazi kwamba Iran inatakiwa kupunguza mpango wake wa nyuklia kwa matumizi ya raia kwa masharti ya kufutiwa hatua kwa hatua vikwazo vya kimataifa.

Lakini utawala wa Rais Donald Trump, ambao unapinga mkataba huo uliafikiwa na mtangulizi wake Barack Obama, uliweka vikwazo vya kisheria na kifedha kwa Iran, visvyohusiana na shughuli za nyuklia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.