Pata taarifa kuu
KOREA KASKAZINI-MAREKANI-USALAMA

Moon Jae-in: Hakuna hatua za kijeshi bila ridhaa ya Seoul

Rais wa Korea Kusini Moon Jae-in amesema Jumanne hii kuwa kutakuwa na hatua za kijeshi kwenye penesula ya Korea bila ridhaa ya Seoul na kuoongeza kuwa serikali yake itajitahidi kuepuka vita kwa njia zote.

rais wa Korea Kusini Moon Jae-in.
rais wa Korea Kusini Moon Jae-in. REUTERS/Kim Hong-Ji
Matangazo ya kibiashara

Peninsula ya Korea inakabiliwa na mvutano kutokana na harakati za Korea ya Kaskazini kuendelea na mpango wake nyuklia, uliyosababisha kuongezeka kwa vita vya maneno kati ya Korea Kaskazini na Marekani, ambayo ni msirika wa karibu wa Korea Kusini.

"Hatua ya kijeshi kwenye Peninsula ya Korea inaweza tu kuamuliwa na Korea ya Kusini na hakuna mtu mwingine anaweza kuamua kuchukua hatua za kijeshi bila ridhaa ya Korea ya Kusini," amesema Moon Jae-in katika hotuba inayodhimisha miaka 72 ya kutamatika kwa uwepo wa majeshi ya Japan kwenye peninsula hiyo kuanzia mwaka 1910 hadi 1945.

"Serikali itazuia vita kwa njia zote," Moon Jae-in aliongeza.

Alitoa wito kwa Korea ya Kaskazini kuketi kwenuye meza ya mazungumzo, akibaini kwambavikwazo vilivyochukuliwa dhidi yake vililenga kuishinikiza kwenda kwenye mezaya mazungumzo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.