Pata taarifa kuu
KOREA KASKAZINI-MAREKANI-USALAMA

Kim Jong-un: Nasubiri kuona mtazamo wa Marekani kabla ya kuchukua hatua

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un anasema anasubiri kuona mtazamo wa Marekani kabla ya kuchukua uamuzi kuhusu uwezekano wa kurusha makombora kuelekea karibu na kisiwa cha Marekani cha Guam, shirika la habari la Korea ya Kaskazini, KCNA limearifu Jumanne hii.

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un.
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un. KCNA/via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Akionekana kwa mara ya kwanza tangu wiki mbili zilizopita, Kim Jong-un alitembelea uongozi wa kmajeshi siku ya Jumatatu na alitathmini mpango wake wa kurusha makombora kuelekea katika kisiwa cha Guam, kwa mujibu wa KCNA.

Wakati huo huo rais wa Korea Kusini Moon Jae-in amesema Jumanne hii kuwa kutakuwa na hatua za kijeshi kwenye penesula ya Korea bila ridhaa ya Seoul na kuoongeza kuwa serikali yake itajitahidi kuepuka vita kwa njia zote .

Korea Kaskazini na Marekani wamekua wakiendelea katika vita vya maneno kwa miezi kadhaa sasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.