Pata taarifa kuu
URUSI-MAREKANi-VIKWAZO

Urusi yaishtumu Marekani kutangaza ''vita vya kibiashara dhidi yake

Serikali ya Urusi kupitia Waziri wake Mkuu Dmitry Medvedev amelaani kuwa vikwazo vipya vilivyowekwa na Marekani dhidi ya nchi hiyo akisem akuwa ni sawa na kutangaza vita vya kibiashara dhidi ya Urusi.

Rais wa Urusi Vladimir Putin na Waziri wake Mkuu Dmitry Medvedev wakimuonya rais wa Marekani Donald Trump..
Rais wa Urusi Vladimir Putin na Waziri wake Mkuu Dmitry Medvedev wakimuonya rais wa Marekani Donald Trump.. REUTERS/Dmitry Astakhov/Sputnik
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Marekani Donald Trump ameusaini kuwa sheria mswada ambao utaiwekea vikwazo vipya Urusi, kwa kuingilia katika uchaguzi wa Marekani mwaka 2016. Uamuzi huo umechukuliwa baada ya Baraza la Seneti la Marekani kuidhinisha vikwazo hivyo licha ya pingamizi la awali la White House.

Sheria hiyo inalenga kuiadhibu Urusi kwa kuingilia uchaguzi wa Marekani wa 2016 pamoja na vitendo vyake dhidi ya Ukraine.

Bw Medvedev amesema kuwa mikakati iliotiwa saini na rais Trump inaonyesha udhaifu wa rais huyo wa Marekani ambaye alisema ameaibishwa na bunge la Congress.

Bwana Medvedev pia alionya kwamba hatua mpya zinazolenga kumuondoa rais Trump madarakani zitachukuliwa kwa kuwa sio mtu aliye na utaratibu.

Mswada huo pia unaziwekewa viwazo Iran na Korea Kaskazini.

Iran imesema kuwa vikwazo hivyo vipya vinakiuka makubaliano ya mpango wa nyukliahuku ikibaini kwamba itajibu kwa njia ilio ''sahihi'' kwa mujibu wa shirika habari la Isna.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.