Pata taarifa kuu
MAREKANI-URUSI-USHIRIKIANO

Putin: wanadiplomasia 755 wa Marekani watakiwa kuondoka Urusi

Rais wa Urusi Vladimir Putin ametoa agizo kwa wanadiplomasia 755 wanaohudumu kwenye ubalozi wa Marekani nchini Urusi kuondoka katika ardhi ya Urusi kufikia Septemba mosi.

Rais wa Urusi Vladimir Putin aionya Marekani.
Rais wa Urusi Vladimir Putin aionya Marekani. REUTERS/Sergei Karpukhin
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii ya Urusi imekuja baada ya vikwazo vipya dhidi ya Urusi kuidhinishwa kwa wingi wa kura na baraza mbili za bunge nchini Marekani siku ya Jumanne, licha ya pingamizi la Ikulu ya White house.

Marekani kwa upande wake, inasema imesikitishwa na uamuzi huo, na inapima athari na kutafakari namna ya kujibu hatua hiyo

Urusi imeidhinisha hatua hiyo kwa ghadhabu kufuatia vikwazo vipya vilivyopitishwa na bunge la Marekani dhidi yake, kwa tuhuma za kuingilia uchaguzi wa taifa hilo mwaka jana.

Rais Vladimir ameapa kuwa upo uwezekano wa kuongeza vikwazo zaidi dhidi ya serikali ya Marekani.

Rais Putin alisema kuwa alitarajia uhusiano baina ya Moscow na Washington ungebadilika na kuwa mzuri, lakini hilo haliwezekani kwa sasa.

Wakati huo huo Makamu wa rais wa Marekani, Mike Pence, alisema ana imani kwamba tabia ya serikali ya Urusi itabadilika.

Mwaka uliopita rais Obama aliamuru kutimuliwa kwa wanadiplomaisa 35 wa Urusi kufuatia tuhuma za Urusi kutaka kuingilia katika uchaguzi wa Marekani kupitia njia ya mtandao.

Makazi ya wanadiplomasia wawili wa Urusi yalifungwa na baadae kuwekewa vikwazo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.