Pata taarifa kuu
KOREA KASKAZINI-MAREKANI

Korea Kaskazini yasema makombora yake yanaweza kufika Marekani

Korea Kaskazini inasema imefanikiwa kurusha kombora la masafa marefu, na kusema ni onyo kwa Marekani.

Jaribio la kombora la Korea Kaskazini
Jaribio la kombora la Korea Kaskazini Reuters/路透社
Matangazo ya kibiashara

Kiongozi wa nchi hiyo Kim Jong-un, amesema jaribio hili linaonesha uwezo wa kuishambulia Marekani.

Rais Donald Trump amelaani jaribio hili na kusema halikubaliki kamwe.

China ambayo imekuwa mshirika wa karibu wa Korea Kaskazini, pia imelaani hatua hii ambayo inakwenda kinyume na azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani Rex Tillerson amesema China na Urusi, zinawajibikia mwendelezo wa majaribio na vitisho hivi vya Korea Kaskazini.

China pamoja na kwamba, imekuwa ikilaani majaribio haya, imekuwa ikitaka Marekani na Korea Kaskazini na nchi jirani kama Japan na Korea Kusini kuja kwenye meza ya mazungmzo na kujadili suala hili.

Urusi nayo imekuwa ikisema kuwa Jumuiya ya Kimataifa haistahili kuwa na wasiwasi kuhusu majaribio haya ya Korea Kaskazini.

Rais Trump ameonya mara kwa mara kuwa nchi yake iko tayari kuishambulia Korea Kaskazini ikiwa itaendeleza majaribio haya.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.