Pata taarifa kuu
CHINA-XIAOBO-HAKI

Mshindi wa tuzo ya Nobel China, Liu Xiaobo, afariki dunia

Mshindi pekee wa tuzo ya amani ya Nobel nchini China pia mpinzani mkuu nchi humo, Liu Xiaobo, ameaga dunia Alhamisi hii akiwa na umri wa miaka 61 katika hospitali ya Shenyang.

Liu Xiaobo, Mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel.
Liu Xiaobo, Mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel. DANIEL SANNUM LAUTEN / AFP
Matangazo ya kibiashara

Kifo chake kimetokea saa 48 tu baada ya kuondolewa gerezani na kupelekwa hospitalini, kwa matibabu ya maradhi ya saratani ya ini.

Liu Xiaobo alikuwa akitumikia kifungo cha miaka 11 jela, kwa kosa la kusambaza shinikizo kwenye mitandao, akitoa wito kwa China kukomesha utawala wa chama kimoja cha kisiasa.

Liu Xiaobo alikuwa mwaandishi na mwanasiasa, msomi mwenye sifa kubwa, ambaye daima alikuwa akishinikiza kuwepo kwa mabadiliko ya amani ya kisiasa.

Itakumbukwa kwamba Bw Xiaobo alikuwa mmojawepo wa mshirika mkuu wa wanaounga mkono kuwepo kwa maandamano ya demokrasia katika uwanja wa Tiananmen Square mnamo mwaka 1989.

Wanaharakati wa haki za kibinadamu na nchi mbalimbali duniani hasa zile za Magharibi, yamekuwa yakitoa wito kwa China kumruhusu mwanasiasa huyo mkongwe kwenda nje ya nchi kwa matibabu, bila mafanikio.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.