Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 24/03 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 23/03 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 23/03 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Asia

China: Nguvu za kijeshi dhidi ya Korea Kaskazini sio suluhu

media Liu Jieyi, Balozi wa China kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, alisema kuwa kupelekwa kwa makombora na vifaa vingine vya kuzuia makombora kutoka Marekani nchini Korea Kusini katika miezi ya hivi karibuni, imechangia kupanda kwa mvutano katika ka REUTERS/Mike Segar

China kupitia balozi wake kwenye Umoja wa Mataifa Liu Jieyi, alisema katika kikao cha dharura cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwamba chaguo la kutumia nguvu za kijeshi dhidi ya Korea Kaskazini halina nafasi wakati huu.

Bw Jieyi alitoa kauli hiyo akijibu hoja iliyotolewa na Marekani kupitia baloze wake katika umoja huo Nikki Haley kwamba nguvu za kijeshi zitatumiwa dhidi ya Korea Kaskazini kama itahitajika.

Mvutano huo unaibuka siku mbili tu baada ya Korea Kaskazini kufanyia majaribio kombora lake la masafa marefu la ICBM linalorushwa kutoka bara moja kwenda jingine.

Liu Jieyi alirejelea wito wa China na Urusi kwa Korea Kaskazini kusitisha majaribio ya makombora iwapo Marekani na Korea Kusini zitasitisha mazoezi ya pamoja ya kijeshi.

Awali baloxi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa Nikki Haley alisema kuwa vitendo vya Korea Kaskazini ni ishara za kuzuka kwa mgogoro duniani, na mpango wake wa kurusha makombora ya masafa marefu unalenga kuhatarisha usalama wa Marekani na wa dunia.

Wakati huo huo Waziri wa Ulinzi wa Marekani James Mattis na mwenzake wa Japan Tomomi Inada walisema kuwa jaribio hilo ni uchokozi ambao hautakubalika.

Korea Kaskazini ilifanya jaribio hilo ambalo linakiuka marufuku ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, licha ya vitisho vya Marekani na Umoja wa Mataifa.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana