Pata taarifa kuu
MAREKANI-KOREA KASKAZINI-CHINA-USALAMA

Trump aishtumu China kwa kufanya biashara na K. Kaskazini

Rais wa Marekani Donald Trump ameilaumu China kuendelea kufamya biashara na Korea Kaskazini kufuatia uamuzi wa Korea Kaskazini kutekeleza jaribio la kombora la masafa marefu.

Marekani imesema jaribo jipya la Korea Kaskazini ni tishio kwa usalama wake na wa dunia.
Marekani imesema jaribo jipya la Korea Kaskazini ni tishio kwa usalama wake na wa dunia. U.S. Department of Defense, Missile Defense Agency/Handout via R
Matangazo ya kibiashara

Marekani imetaka kufanyika kwa mkutano wa dharura wa baraza la ulinzi la Umoja wa Mataifa kujadili suala hilo.

Wakati huo huo China na Urusi wameitakaMarekani na Korea Kaskazini kuacha kuonyesha ubabe wao wa kijeshi na kusema wanapinga majaribio yoyote ya kubadilisha uongozi nchini Korea Kaskazini.

Marekani inasema Jaribio la kombora la hivi la siku ya Jumanne lilienda kinyume na marufuku ya baraza la ulinzi la Umoja wa Mataifa.

China ambaye ni mshirika mkubwa wa kiuchumi wa Korea Kaskazinia na Urusi, imetaka Korea Kaskazini kuachana na progamu yake ya makombora ya masara marefu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.