Pata taarifa kuu
MAREKANI-KOREA KASKAZINI-USALAMA

Meli ya kivita ya Marekani yawasili Kora Kusini

Meli ya kivita ya Marekani imeegesha katika rasi ya Korea Kusini, wakati huu kukiwa na hofu kuwa huenda Korea Kaskazini ikajaribu tena makombora yake ya silaha za Nyuklia.

Ndege ya kivita ya Marekani USS Carl Vinson imeegesha katika rasi ya Korea Kusini.
Ndege ya kivita ya Marekani USS Carl Vinson imeegesha katika rasi ya Korea Kusini. REUTERS/Mike Blake
Matangazo ya kibiashara

Hatua ya Marekani kutuma meli hii ya kivita imekuja wakati huu Korea Kaskazini ikiadhimisha miaka 85 tangua kuanzishwa kwa jeshi lake hivi leo.

Hivi karibuni kumekuwa na hali ya wasiwasi kati ya Marekani na Korea Kaskazini, nchi zote ambazo zimekuwa zikitishia kushambuliana na kuzua pia hali ya wasiwasi katika nhi jirani kama Japan, China na Korea Kusini.

Meli hizo zilitumwa na Rais Donald Trump baada ya onyo kuhusu uvumilivu kumalizika dhidi ya mpamgo ya nuklia ya Korea Kasakazini.

Mwishoni mwa wiki iliyopita Korea Kaskazini ilitangaza kuwa iko tayari kuzamisha meli ya kubeba ndege ya Marekani inayoelekea rasi ya Korea.

Taarifa katika gazeti la Rodong Sinmun lilisema kuwa meli ya Marekani ya USS Carl Vinson itazamishwa kwa shambulizi moja.

Gazeti la Rodong Sinmum limesema "vikosi vyetu viko tayari kuzamisha meli hiyo ya kubeba ndege ya Marekani kwa shambulizi moja tu".

Vita vya maneno viliibuka baada tu ya Marekani kuionya Korea Kaskazini kutoendelea kufanya majaribio ya makombora ya masafa marefu pamoja na kuendeleza mpango wake wa nyuklia.

Korea Kaskazini iliapa kuendelea na mpango wake pamoja na majaribio ya makombora kila wiki na kila mwezi kwa minajili ya usalam wake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.