Pata taarifa kuu
MAREKANI-JAPAN-KOREA KASKAZINI-USALAMA

Marekani na Japan kuishinikiza Korea Kaskazini kuachana na mpango wake wa nyuklia

Viongozi wawili kutoka Marekani na Japan ambao ni Makamu wa Rais wa Marekani Mike Pence na naibu Waziri mkuu wa Japan Taro Aso, wameafikiana kuishinikiza Korea Kasikazini kuachana na mpango wake wa silaha za Nyuklia.

Makamu wa rais wa Marekani Mike Pence katika mji wa Paju, Aprili 17, 2017.
Makamu wa rais wa Marekani Mike Pence katika mji wa Paju, Aprili 17, 2017. REUTERS/Kim Hong-ji
Matangazo ya kibiashara

Makamu wa Rais wa Marekani Mike Pence amesema Marekani itaendelea kushirikiana na Japan na washirika wengine katika ukanda na China, kuweka vikwazo vya kidplomasia na kiuchumi dhidi ya Korea Kaskazini,ili iachane na mpango wake wa silaha za nyuklia. Licha ya kauli hiyo mapendekezo yote yanaendelea kujadiliwa.

Bw Pence amesema Marekani ina amini kuwa njia yenye mafanikio ni mazungumzo ya kimataifa kuishinikiza na kuitenga Korea Kaskazini kutokana na msimamo wake, lakini amesisitiza kuwa njia zote zina uzito wake.

kuweka msukumo wa Kidiplomasia na kiuchumi dhidi ya
Kwa upande wake rais wa Japan Shinzo Abe amemwambia Mike Pence kuwa Japan inataka kufikia makubaliano kwa njia ya majadiliano wala sio kwa njia ya vita.

Japan imetaka Marekani kutotumia nguvu za kivita ili kuishawishi Korea Kaskazini kuachana na mpango wake wa nyuklia.

"Kimsingi tunatakiwa kuwa na njia ya amani kuhusiana na jambo hili, hata kama mazungumzo kama kwa jambo hili hayana maana.Ni muhimu kwetu kutumia nguvu dhidi ya Korea Kaskazini kuihusisha kuishawishi kuachana na mpango wake wa nyuklia, " amesema rais wa Japan Shinzo Abe.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.