Pata taarifa kuu
KOREA KASKAZINI-MAREKANI-USALAMA

Korea Kaskazini yaapa kuendelea na majaribio yake kila wiki

Serikali ya Korea Kaskazini imeapa kuendelea kufanya majaribio ya makombora yake kila wiki, licha ya vitisho vya Umpja wa Mataifa hasa Marekani ambayo imekua ikiinyooshea kidole cha lawama.

Rais wa Korea Kaskazini Kim Jong-un, mjini Pyongyang, Aprili 13, 2017.
Rais wa Korea Kaskazini Kim Jong-un, mjini Pyongyang, Aprili 13, 2017. Ed JONES / AFP
Matangazo ya kibiashara

Maafisa wa usalama wa Korea Kaskazini wamesema Korea Kaskazini itaendelea kufanya majaribio yake kwa mnajili ya usalama wake.

''Tutakua tukifanya majaribio zaidi kila wiki, kila mwezi na kila mwaka '', Naibu Waziri wa masuala ya kigeni Han Song-ryol ameesema.

Mapema wiki hii Makamu wa rais wa Marekani, Mike Pence aliionya Korea Kaskazini kutoijaribu Marekani.

Muda wa kuivumilia Korea Kaskazini kwa miaka mingi umekwisha na hatutokubali kuendelea kufumbia macho inayoyafanya ambayo ni kinyume na sheria za kimataifa, “ amesema Mike Pence.

Hali ya wasiwasi imekuwa ikiongezeka katika eneo la Peninsula, wakati huu kukiwa na hali ya kushambuliana kwa maneno baina ya Korea kaskazini na Marekani.

Bwana Han amesema ikiwa Marekani inapanga kutekeleza shambulio la kijeshi dhidi Korea Kaskazini, kuna uwezekano twachukuwe hatua ya kupambana kwa shambulio la Nuklia kwa mbinu zao na mtindo wao.

Mike Pence aliwasili nchini Korea Kusini mwishoni mwa juma lililopita baada ya Kombora la Korea kaskazini kushindwa kupaa angani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.