Pata taarifa kuu
UTURUKI

Raia wa Uturuki kupiga kura ya mabadiliko ya katiba siku ya Jumapili

Kampeni za kura ya maoni nchini Uturuki zimeingia katika dakika za lala salama kuelekea upiga  kura siku ya Jumapili.

Bango la kampeni ya kura hii ya maoni jijni Istanbul
Bango la kampeni ya kura hii ya maoni jijni Istanbul REUTERS/Murad Sezer
Matangazo ya kibiashara

Raia wa Uturuki watapiga kura kuamua ikiwa waibadilishe katiba ya nchi hiyo ili kuondoa wadhifa wa Waziri Mkuu na mfumo wa uongozi wa bunge.

Ikiwa raia wa Uturuki watafanikiwa katika mabadiliko hayo ya pengele 18, basi rais atakuwa na mamlaka makubwa ikilinganishwa na ilivyo sasa.

Pamoja na hilo, inapendekezwa kuwa idadi ya wabunge bungeni iongezwe kutoka 550 hadi 600.

Kura za maoni zinaonesha kuwa upande wowote unaweza kushinda kura hii ya maoani.

Rais Recep Tayyip Erdogan anaunga mkono mabadiliko haya ya katiba na amekuwa akitoa wito kwa raia wa nchi hiyo kuunga mkono mabadiliko hayo.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.