Pata taarifa kuu
CHINA

Amnesty International yasema China bado inaongoza katika utoaji wa adhabu ya kunyongwa

Shirika la Kimataifa la kutetea haki za Binadamu duniani la Amnesty International linasema China linasalia taifa pekee duniani linaloongoza katika utekelezwaji wa adhabu ya kunyongwa.

Picha ikionesha namna hukumu ya kunyongwa inavyotekelezwa
Picha ikionesha namna hukumu ya kunyongwa inavyotekelezwa Amnesty International
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo, shirika hilo linasema idadi ya watu walionyongwa mwaka 2016 katika mataufa mbalimbali duniani.

Watu 1,032 walinyongwa katika mataifa mbalimbali duniani mwaka uliopita, idadi ambayo inaelezwa imeshuka kwa asilimia 35 ikilinganishwa  na mwaka 2015.

Amnesty bila kueleza idadi kamili, inasema mami ya watu mwaka uliopita, walinyongwa nchini China wakiwemo raia wa kigeni.

Mbali na China, mataifa mengine yanayoongoza katika utekelezwaji wa adhabu hii ni pamoja Iran, Saudia Arabia, Iraq na Pakistan.

Hata hivyo kwa mara ya kwanza, idadi ya kwanza Marekani iliwanyonga watu 20, idadi inayoelezwa kuwa ndogo zaidi nchini humo tangu mwaka 1991.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.