Hong Kong ilijitenga tangu ilipokabidhiwa mikononi mwa China baada ya kutawaliwa na wakoloni waingereza mwaka 1997.
Hata hivyo miaka 20 baadae kumekuwa na wasiwasi kuwa Beijing haitambui mkataba wa makabidhiano uliobuniwa kulinda uhuru wa Hong Kong.
Mtumishi wa zamani wa umma aliyechaguliwa kuwa kiongozi mkuu na kamati inayounga mkono China alionekana kuwa chaguo la Beijing kuongoza.
Wakosoaji wanasema atazidisha mgawanyiko katika mji huo licha ya Lam kuahidi kuiunganisha Hong Kong.