Pata taarifa kuu
KOREA KASKAZINI-JAPAN-USHIRIKIANO

Korea kaskazini yarusha makombora katika bahari ya Japan

Jeshi la Korea kusini, Korea kaskazini imerusha makombora yake kadhaa katika bahari ya Japan. Kwa mujibu wa jeshi la Korea kusini makombora hayo yamerushwa kutoka kwenye eneo la Tongchang-ri lililo kwenye mpaka kati ya Korea kaskazini na China na kurushwa kwa umbali wa takriban kilomita elfu moja.

Aina ya makombora ya Scud-B ya Korea Kaskazini yaliyoonyeshwa mjini Seoul. Korea Kusini inahofia kwamba aina hii ya makombora ndio yamerushwa nchini Japan.
Aina ya makombora ya Scud-B ya Korea Kaskazini yaliyoonyeshwa mjini Seoul. Korea Kusini inahofia kwamba aina hii ya makombora ndio yamerushwa nchini Japan. REUTERS/Lee Jae-Won
Matangazo ya kibiashara

Katika mkutano na waandishi wa habari, Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe amesema makombora hayo yanadhihirisha ushahidi tosha wa vitisho vipya kutoka Korea kaskazini

''Korea kaskazini imefyatua makombora yake manne leo na kuangukia karibu na eneo letu la maji lenye manufaa kwetu kiuchumi, “ amesema Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe.

Bw Abe ameongeza kuwa Japan itakusanya taarifa na kuzichambua kuhusu tukio hili.

"Inaonyesha wazi kuwa Korea kaskazini ni tishio jipya kufuatia makombora yaliyorushwa wakati huu katia eneo letu. Korea kaskazini ilitangaza kuwa na aina hii mpya ya makombora na sasa imetekeleza ahadi yake ya kuyarusha katika moja ya eneo letu, tutafuatilia suala hili kwa umakini mkubwa, '' amesisitiza Bw Abe, kabla ya kusema Japan inaipinga vikali Korea kaskazini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.