Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 05/12 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 05/12 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 05/12 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Habari mpya kabisa
  • Marekani: Spika wa Baraza la Congress Nancy Pelosi atoa wito wa kuandaa mashtaka dhidi ya Trump kwa ajili ya ung'atuzi
Asia

Wanawake wawili wahusishwa na kifo cha Kim Jong Nam

media Maandamano nje ya ubalozi wa Korea Kaskazini kupinga dhidi ya mauaji ya ndugu wa kambo wa kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-nam, 13 Februari. REUTERS/Athit Perawongmetha

Wanawake wawili waliokamatwa kwa madai ya kuhusika na kifo cha ndugu wa kambo wa kiongozi wa Korea Kaskazini, watafunguliwa mashtaka ya kuhusika na kifo cha Kim Jong-nam nchini Malaysia.

Jaji mkuu wa Mahakama ya nchini Malaysia, amesema wanawake hao wawili mmoja akijulikana kwa jina la Siti Aisyah, mwenye umri wa 25, kutoka Indonesia na mwingine Doan Thi Huong, mwenye umri wa 28, kutoka Vietnam wanadaiwa kumuua ndugu wa kambo wa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Nam watajibu mashtaka dhidi yao kwa kutumia sumu kali kuuwa katika uwanja wa ndege mjini Kuala Lumpar.

Wanawake hao ni miongoni mwa watu kumi ambao wanashukiwa na Malaysia kwamba huenda walihusika na mauaji hayo.

Vyanzo vya kisheria nchini Malaysia vimesema wanawake hao watashtakiwa chini ya sheria ya nchi na iwapo watapatikana na hatia watanyongwa.

Malaysia inasema, Bwana Kim aliyekuwa mkosoaji wa nduguye, aliuwawa kwa kutumia sumu kali ambayo imepigwa marufuku na Umoja wa mataifa.

Washukiwa hao wawili wanadaiwa kumpaka usoni kemikali hiyo ya sumu katika uwanja wa ndege wa Malaysia mapema mwezi huu.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana