Pata taarifa kuu
KOREA KASKAZINI-MALAYSIA

Malaysia yamwagiza Balozi wake nchini Korea Kaskazini kurudi nyumbani

Mzozo wa kidiplomasia umezuka kati ya Korea Kaskazini na Malaysia kutokana na kifo cha Kim Jong-nam, kaka wa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un.

Kim Jong-nam akiwa katika uwanja wa ndege jijini Kuala Lumpur kabla ya kuuawa
Kim Jong-nam akiwa katika uwanja wa ndege jijini Kuala Lumpur kabla ya kuuawa Kyodo/via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Malaysia imemwondoa Balozi wake kutoka jijini Pyongyang na kumrudisha nyumbani na kumwita Balozi wa Korea Kaskazini ili kumhoji anachokifahamu kuhusu kifo hicho.

Kim Jong Nam, aliuawa katika mazingira ya kutatanisha akiwa katika uwanja wa ndege wa Kuala Lumpur.

Polisi nchini humo wanawahoji washukiwa watatu waliokamatwa kwa madai ya kuhusika na kifo hicho.

Inaaminiwa kuwa, Kim Jong Nam alipewa sumu, iliyosababisha kifo chake.

Korea Kusini imeishutumu Korea Kaskazini mwa kuhusika moja kwa moja na kifo hicho.

Serikali nayo Korea Kaskazini nayo imeishutumu Malaysia kwa kuwapa hifadhi maadui wa nchi yao.

Pyongyang imetaka mwili Kim Jong Nam kurejeshwa nchini mwao.

Malaysia imesema haiwezi kufanya hivyo hadi pale uchunguzi utakapomalizika lakini pia vinasaba za familia yake kuchunguzwa.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.