Pata taarifa kuu
URUSI-UN-KIFO

Balozi wa Urusi katika Umoja wa Mataifa Vitaly Churkin afariki ghafla

Balozi wa Urusi katika Umoja wa Mataifa, Vitaly Churkin, amefariki "ghafla" mjini New York Jumatatu wiki hii, Wizara ya mambo ya Nje ya Urusi imetangaza, bila hata hivyo kufafanua sababu ya kifo chake.

Vitaly Churkin, Oktoba 6, 2016 katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York.
Vitaly Churkin, Oktoba 6, 2016 katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York. AFP
Matangazo ya kibiashara

"Mwakilishi wa kudumu wa Urusi katika Umoja wa Mataifa, Vitaly Churkin, amefariki ghafla mjini New York Februari 20," Wizara ya Mambo ya Nje imesema katika taarifa yake.

Churkin amefariki siku moja kabla ya siku yake ya kuzaliwa ya miaka 65, Wizara ya mambo ya Nje ya Urusi imeongeza.

"Mwanadiplomasia huyo mahariamefariki akiwa bado anahudumu," wizara ya mambo ya Nje ya Urusi imebaini katika taarifa yake.

mwakilishi wa Urusi alikuwa katika nafasi hiyo tangu mwaka 2006. Awali alifanya kazi katika Wizara ya Mambo ya Nje mjini Moscow. Aliwahi kuwa balozi wa Urusi nchini Canada, Ubelgiji na mwakilishi maalumu wa Urusi katika mazungumzo kuhusu Yugoslavia ya zamani (1992-1994).

Wanadiplomasia waliokuwa wakifanya mkutano katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York walisalia kimya kwa muda wa dakika moja kwa wakati wa tangazo la kifo chake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.