Pata taarifa kuu
KOREA KASKAZINI-MALAYSIA

Korea Kaskazini na Malaysia walumbana kuhusu kuuawa kwa Kim Jong Nam

Korea Kaskazini imesema haitakubali, matokeo ya ripoti itakayotolewa na serikali ya Malaysia kueleza kilichosababisha kifo cha Kim Jong Nam.

Polisi wakizingira eneo ambalo Kim Jong Nam alikouliwa
Polisi wakizingira eneo ambalo Kim Jong Nam alikouliwa REUTERS/CCTV
Matangazo ya kibiashara

Jong Nam ni kaka wa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong un.

Aliuawa mapema wiki hii akiwa katika uwanja wa ndege jijini Kuala Lumpur.

Kumekuwa na ripoti kuwa Kim Jong Nam alipoteza maisha baada ya kupewa sumu na mwanamke mmoja na uchunguzi kuhusu madai haya unaendelea.

Tayari Korea Kaskazini imesema inataka mwili Kim Jong Nam urejeshwe nyumbani lakini Malaysia imekataa na kusema inaweza kufanya hivyobaada ya kufanya uchunguzi wa vinasaba kutoka kwa familia yake.

Siku ya Jumamosi Polisi nchini Malaysia wamesema wamemkamata Ri Jong Chol, raia wa Korea Kaskazini anadaiwa kuhusika na kifo cha Jong Nam.

Pyongyang imeishutumu Malaysia kwa kuwapa hifadhi maadui wa taifa lake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.