Pata taarifa kuu
KOREA KASKAZINI-MALAYSIA

Mshukiwa wa mauaji ya ndugu wa kambo wa Kim Jong-un akamatwa

Mamlaka nchini Malaysia imemkamata mwanamke mmoja kutoka Burma kama sehemu ya uchunguzi wa mazingira ya kifo cha ndugu wa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un, limearifu Jumatano shirika la habari la Malaysia la Bernama.

Kim Jong-Nam (kushoto), mtoto wa kiongozi wa mwisho wa Korea Kaskazini Kim Jong-Il, na ndugu yake wa kambo, ambaye ni kiongozi wa sasa wa Korea Kaskazini Kim Jong-Un (kulia).
Kim Jong-Nam (kushoto), mtoto wa kiongozi wa mwisho wa Korea Kaskazini Kim Jong-Il, na ndugu yake wa kambo, ambaye ni kiongozi wa sasa wa Korea Kaskazini Kim Jong-Un (kulia). Toshifumi KITAMURA, Ed JONES / AFP
Matangazo ya kibiashara

Mwanamke huyo amekamatwa katika uwanja wa ndege wa Kuala Lumpur unaotumiwa na mashirika ya ndege ya gharama nafuu, shirika hilo limesema likimnukuu afisa mwandamizi wa polisi.

Hakuna maelezo zaidi ambayo yametolewa kwa sasa na polisi ya Malaysia haijazungumza lolote mpaka sasa.

Korea ya Kusini inawashuku wanawake wawili ambao ni maafisa wa Idara ya ujasusi ya Korea Kaskazini kuwa ndio walimpa sumu Kim Jong-nam, ndugu wa kambo wa Kim Jong-un Jumanne katika uwanja wa ndege wa Kuala Lumpur, kwa amri ya kiongozi wa Korea Kaskazini.

Kim Jong-nam, ambaye alikuwa akiondoka katika mji wa Macau, alijisika vibaya kiafya katika uwanja huo wa ndege na kifo chake kilitokea wakati aliposafirishwa hospitalini, polisi ya Malaysia imesema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.