Pata taarifa kuu
UNSC-KOREA KASKAZINI-USALAMA

UNSC yalaani jaribio jipya la Korea Kaskazini

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lililokutana kwa dharura Jumatatu, Februari 13 kwa ombi la Washington, Tokyo na Seoul, kufuatia kitendo cha Korea Kaskazini cha kurusha kombora la masafa marefu lijulikanalo kama Fter Its Ballistica.

Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Nikki Haley, Januari 27, 2017 katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York.
Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Nikki Haley, Januari 27, 2017 katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York. REUTERS/Mike Segar
Matangazo ya kibiashara

Wanadiplomasia walilaani kwa kauli moja kitendo hicho ambacho kinakiuka maazimio ya Umoja wa Mataifa. Lakini ni hasa msimamo wa Beijing, mshirika wa jadi wa Pyongyang, ambayo alikuwa akichunguzwa.

Licha ya jumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kutolewa kwa kauli moja, mabalozi wa baraza hilo walipinga kuomba kwamba vikwazo ambavyo tayari kupigiwa kura dhidi ya Pyongyang viweze kutekelezwa kwa kina.

Nikki Haley, balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa alituma taarifa fupi baada ya mkutano huo. "Wakati umewadia wa kuitaka Korea Kaskazini iwajibike, si kwa maneno tu bali kwa vitendo," Nikki Haley alisema. Pyongyang "na washirika wake" wanapaswa kuelewa kuwa majaribio haya hayakubaliki.

Hatua kali

Mapema mchana, Donald Trump aliahidi kuchukua hatua kali kufuatia kitendo hiki cha Korea Kaskazini.

Trump alitoa matamshi hayo alipokuwa akizungumza na waandishi habari akiwa pamoja na waziri mkuu wa nchi ya Canada, Justin Trudeau katika ikulu ya Marekani, Trump amesema kwamba ataishughulikia na nchi ya akizungumza kwa msisitizo juu ya kauli hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.