Pata taarifa kuu
KOREA KASKAZINI-MAREKANI-USHIRIKIANO

Vita vya maeneno vyaibuka kati ya Trump na Korea Kaskazini

Korea Kaskazini inasema tamko la rais mteule wa Marekani Donald Trump kuwa Korea Kaskazini haina uwezo wa kutumia silaha zake za masafa marefu, ni onyo tosha kwa serikali ya Pyongyang.

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un aona kwamba tamko la Donald Trump ni onyo tosha kwa serikali ya Pyongyang.
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un aona kwamba tamko la Donald Trump ni onyo tosha kwa serikali ya Pyongyang. KCNA/ via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Kauli ya Trump kupitia ukurasa wake wa Twitter, ilikuja baada ya kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-Un kusema kuwa nchi yake ipo katika maandalizi ya lala salama kutengeza silaha za kisasa za masafa marefu na kuimarisha uimara wa silaha zake.

Rais mteule wa Marekani, Donald Trump, alipuuzilia mbali madai ya Korea Kaskazini kuwa imeunda Kombora linaloweza kuwasilisha zana za nuklia hadi Marekani.

Bwana Trump aligusia maneno ya kujigamba ya kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un, katika ujumbe wake wa mwaka mpya ambapo alisema kuwa maandalizi ya kombora la aina hiyo yamefikia hatua ya mwisho

Donald Trump ameshutumu China kwa kushindwa kuthibiti mshirika wake Korea Kaskazini na pia akalaumu Beijing kwa kupokea kiasi kikubwa cha pesa na mali kutoka Marekani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.