Pata taarifa kuu
JAPAN-MAREKANI-USHIRIKIANO

Barack Obama na Shinzo Abe watoa rambirambi zao kwa wahanga wa Pearl Harbor

Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe na Rais wa Marekani Barack Obama walitoa salaamu za rambirambi kwa wahanga wa Pearl Harbor Jumanne, Desemba 27, katika kisiwa cha Hawaii, miaka 75 baada ya shambulizi lililoikumba Marekani. Shambulizi ambalo lilifanywa na Japan.

Rais wa Marekani na Waziri Mkuu wa Japan walizuru Jumanne Desemba 27 eneo la kumbukumbu la USS Arizona huko Pearl Harbor.
Rais wa Marekani na Waziri Mkuu wa Japan walizuru Jumanne Desemba 27 eneo la kumbukumbu la USS Arizona huko Pearl Harbor. REUTERS/Kevin Lamarque
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza katika hafla iliyoandaliwa kwenye kituo cha jeshi la majini la Marekani akiwa pamoja na mwenyeji wake Rais Barak Obama, Shinzo Abe amesema “ ksina usemi kutokana na uzito wa ziara yake katika kumbukumbu ya wale wote waliopoteza maisha kutokana na shambulio hilo.

Bw ameishukuru Marekani kwa uvumilivu wake na kuongeza kuwa kitisho cha vita hakitajirudia kamwe.

Kwa upande wake Barack Obama amesema ziara ya Waziri mkuu wa Japan ni ya kihistoria na kubaini kwamba ziara hiyo inakumbusha kuwa hata maumivu makubwa yaliyotokana na vita yanaweza kuleta urafiki na amani ya kudumu.

Bw Obama amesema baada ya vita mahusiano yao yamekuwa ya amani na nchi zilizokuwa katika ukanda wa Asia Pacifik.

Ziara ya Bw Abe inakuja miezi saba baada ya viongozi hao wawili kuzuru pia mji wa Japan, Hiroshima, ambako Marekani uliushambulia kwa mabomu ya nyuklia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.