Pata taarifa kuu
BURMA-USALAMA

Ukandamizaji na mgogoro wa kibinadamu katika jimbo la Arakan

Ukandamizaji unaendelea katika jimbo la Arakan, nchini Burma. watu 15,000 wameyakimbia makazi yao tangu jeshi kudhibiti eneo la mpakani na Bangladesh. Maelfu ya watu wengine bado wanakabiliwa na mateso yanayotekelezwa na askari.

Polisi ya Burma yapiga doria magharibi mwa nchi.
Polisi ya Burma yapiga doria magharibi mwa nchi. REUTERS/Stringer
Matangazo ya kibiashara

Jeshi linashtumu baadhi ya watu kutoka jamii ya waislamu ambao ni wachache ya Rohingya kushambulia vituo vya polisi mapema mwezi Oktoba.

Watu 31 waliuawa kulingana na viongozi wa serikali. Umoja wa Mataifa umeomba kufanyika 'uchunguzi sahihi' kwa mauaji hayo.

jeshi limekua likiendesha mashambulizi ya anga katika jimbo la Arakan. Ripoti zinasema kuwa nyumba na misikiti vimechomwa moto. Kwa mujibu wa baadhi ya mashirika yasiyo ya kiserikali, idadi ya vifo na majeruhi inazidi idadi iliyotolewa na serikali.

"Ukandamizaji unaofanyika leo ni mbaya sana. Hata hivyo jeshi limeendelea kuzuia misaada ya kibinadamu, ambapo wanakijiji 50 000 na watoto 65 000 wamenyimwa haki ya kupata chakula, "amesema Cécile harl wa shirika lisilo la kiserikali la Info Birmanie.

Maelfu ya watu wameyahama makazi yao, baadhi wamesafiri kwa meli, wengine wametumia usafiri wa magari, au kujificha katika vijiji vingine. Hata hivyo hotuba mbalimbali zinazokuza chuki zimekua zikitolewa na baadhi ya watu dhidi ya Waislamu kutoka jamii ya Rohingya.

"Leo hii katika mitaa ya mji waRangoon tunasikia vitisho vya magaidi wa Kiislamu walio katika jimbo la Arakan, ingawa hakuna habari iliyotolewa kuhusu vurugu hizo," Cécile harl ameendelea.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.