Pata taarifa kuu
UFILIPINO-MAREKANI-USHIRIKIANO

Rais wa Ufilipino Rodrigo Duterte ajutia maneno yake

Jumanne, Septemba 6, Rais wa Ufilipino Rodrigo Duterte ameelezea masikitiko yake baada ya kumkashifu Rais wa Marekani Barack Obama Jumatatu wiki hii akimtaja kuwa ni "mwana wa kahaba."

Rais wa Ufilipino Rodrigo Duterte katika mkutano na waandishi wa habari kabla ya kuondoka kwake kwa ajili ya mkutano wa Asean katika mji wa Laos, Septemba 5, 2016 Davao.
Rais wa Ufilipino Rodrigo Duterte katika mkutano na waandishi wa habari kabla ya kuondoka kwake kwa ajili ya mkutano wa Asean katika mji wa Laos, Septemba 5, 2016 Davao. REUTERS/Lean Daval Jr
Matangazo ya kibiashara

Wakati huo huo Barack Obama amefuta mkutano wake iliyokuwa umepangwa Jumanne hii Septemba 6 na Rais wa Ufilipino Rodrigo Duterte. Uamuzi huo unakuja baada ya rais wa Ufilipino kumtusi hadharani mwenzake wa Marekani.

Mzozo halisi wa kidiplomasia umeendelea kukua kati ya Marekani na mshirika wake Ufilipino katika siku za hivi karibuni. Washington na Manila wanashirikiana hasa katika makubaliano ya kijeshi.

Wakati wa mkutano baina ya viongozi hawa wawili uliyokua umepangwa kufanyika Jumanne hii katika mji wa Laos, Barack Obama alitaka kujadili na mwenzake Duterte kuhusu ukandamizaji dhidi ya madawa ya kulevya uliyosababisha, kwa mujibu wa mashirika ya haki za binadamu, vifo vya watu karibu 2 000 nchini Ufilipino, miongoni mwao watu wengi wasio na hatia.

Rais Rodrigo Duterte, ambaye tayari anajulikana kwa kauli zake mbovu, na sera zake zenye mashambulizi alijibu katika mazungumzo hayo akimuita Obama "mwana wa kahaba."

Rais wa Marekani, akihojiwa na waandishi wa habari, ameonekana kuchukua mambo kifalsafa, akielezea kuwa Rais Duterte alikuwa mtu "mwenye hasira", na angeweza kukutana kama angelikuwa na uhakika wa kukutana na rais wa Ufilipino ili kuzungumzia mambo ya ujenzi wa nchi hizo mbili.

Msemaji wa baraza la taifa la usalama Marekani Ned Price ameambia wanahabari kwamba Bw Obama atakutana na Rais wa Korea ya Kusini Park Geun-hye.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.