Pata taarifa kuu
UFILIPINO-CANADA

Mateka wa pili kutoka Canada anyongwa Ufilipino

Ufilipino umethibitisha leo Jumanne kuuawa kwa raia mmoja kutoka Canada aliyetekwa nyara na kundi la waasi la Kiislam la Abu Sayyaf kusini mwa kisiwa cha nchi hiyo.

Vikosi vya Ufilipino vikiendelea kupambana na kundi la waasi wa Kiislamu la Abu Sayyaf, Oktoba 16, 2014
Vikosi vya Ufilipino vikiendelea kupambana na kundi la waasi wa Kiislamu la Abu Sayyaf, Oktoba 16, 2014 REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Waziri Mkuu wa Canada, Justin Trudeau, alisema jana Jumatatu kuwa inaonekana kuwamateka wa pili kutoka Canada aliuawa mwezi Aprili baada ya kuuawa kwa mtu mwingine aliyetekwa na kundi la Abu Sayyaf.

"Tunalaani vikali mauaji ya kikatili na kipumbavu ya Robert Hall, raia wa Canada, aliyetekwa na kundi la Abu Sayyaf katika eneo la Sulu zaidi ya miezi tisa iliyopita," Rais wa Ufilipino Benigno Aquino amesema katika taarifa yake.

Awali, msemaji wa jeshi la Ufilipino alisema kuwa kichwa cha mateka huyo wa Canada kilipatikana Jumatatu usiku karibu na kanisa Katoliki katika kisiwa hicho.

Mbali na raia hao wawili kutoka Canada, watu wengine wawili, kutoka Norway na Ufilipino bado wanashikiliwa mateka na kundi la Abu Sayyaf tangu kutekwa kwao mwezi Septemba mwaka 2015

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.