Pata taarifa kuu
UTURUKI-IS

Uturuki mlipuko watokea Istanbul, watu kadhaa wajeruhiwa

Watu 11, ikiwa ni pamoja na askari polisi saba na raia 4 wameuawa Jumanne hii asubuhi katika shambulio la bomu lililotegwa ndani ya gari katika kata ya kihistoria ya jijini Istanbul.

Polisi yazingira eneo la shambulio katikati mwa Istanbul.
Polisi yazingira eneo la shambulio katikati mwa Istanbul. © Reuters
Matangazo ya kibiashara

Bomu hilo limelipuliwa wakati gari la polisi limekua likipita karibu na eneo hilo katika kata ya Beyazit, kituo hicho kimebaini.

Shambulio hilo lililotokea katika kata ya Beyazit, ambapo raia wengi hutembelea, limewajeruhi watu 36.

Shambulio hilo limetokea katika siku ya pili ya mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Magari mengi ya wagonjwa na magari ya moto yametumwa katika eneo la mlipuko. Watu watano wamejeruhiwa, kulingana na ripoti ya awali iliyotolewa na shirika la habari la Dogan.

Katika tahadhari ya juu, Uturuki ambayo iko katika tahadhari ya juu, ilikumbwa mwaka huu na mashambulizi ya kujitoa mhanga katika maeneo ya utalii ya mjini Istanbul, mashambuli ambayo yalihusishwa kundi la Islamic State na mashambulizi mawili ya mabomu yaliyotegwa ndani ya magari yaliyodaiwa kutekelezwa na wanamgambo wa Kikurdi. Mashambulizi hayo yaligharimu maisha ya watu wengi.

Mei 12, watu wanane walijeruhiwa na mlipuko wa bomu lililotegwa mdani ya gari karibu na kambi ya kijeshi upande wa mji wa Istanbul.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.