Pata taarifa kuu
INDONESIA-IS-MASHAMBULIZI

Indonesia: IS yakiri kuhusika katika mashambulizi Jakarta

Kundi sla Islamic State limedai kuhusika katika mashambuliziyaliyotokea katika eneo la kati mwa mji wa Jakarta Alhamisi hii. Mashambulizi ambayo yamewaua raia wawili na washambuliaji watano, kwa mujibu wa mamlaka ya Indonesia.

Askari polisi wakikusanyika karibu na maeneo ya mashambulizi katika mji wa Jakarta Januari 14, 2016.
Askari polisi wakikusanyika karibu na maeneo ya mashambulizi katika mji wa Jakarta Januari 14, 2016. REUTERS/Beawiharta
Matangazo ya kibiashara

Mashambulizi haya yamezua hali kubwa ya sintofahamu mjini Jakarta, na kusababisha hofu kwa raia. Baadhi ya raia walihisi mapema kwamba kundi la Islamic State huenda limeanzisha harakati zake katika visiwa vya kusini mashariki mwa Asia.

Zaidi ya washambuliaji wawili wa kujitoa mhanga wamejiliopua katika eneo la kati mwa mji mkuu lenye Ofisi nyingi za mashirika ya Umoja wa Mataifa na balozi mablimbali, ikiwa ni pamoja na ubalozi wa Ufaransa, ambapo milipuko imesikika.

Awali rais, Joko Widodo, alitaja mashambulizi hayo kama vitendo vya "kigaidi" na polisi imetangaza kuwa kundi lenye mafungamano na Islamic State (IS) linashukiwa kutekeleza mashambulizi hayo.

Serikali ya Indonesia ilitangaza wiki chache zilizopita kwamba ilivunja shambulio la kujitoa mhanga lililokua limepangwa na magaidi wenye msimamo mkali, baadhi wakiwa na uhusiano na kundi la IS.

"Magaidi watano wameuawa", Waziri wa usalama wa Indonesia, Luhut panjaitan, amewaambia waandishi wa habari Alhamisi hii mchana, akiongeza kuwa raia mmoja wa Indonesia namwengine kutoka Uholanzi wameuawa katika mashambulizi hayo.

Ubalozi wa Uholanzi haujaithibitisha taarifa hii, ukisema kwamba mmoja wa raia wake amejeruhiwa na amelazwa hospitalini.

Polisi imesema kuwa imedhibiti hali ya mambo na washambuliaji wote wameangamizwa. "Hali kwa sasa imedhibitiwa", amesema Muhammad Iqbal, msemaji wa polisi ya mji wa Jakarta.

Hata hivyo Muhammad Iqbal pia amesema kuwa askari polisi watano, raia mmoja wa kigeni na raia wanne Indonesia wamejeruhiwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.