Pata taarifa kuu
INDONESIA-AJALI-USALAMA

Zoezi la kutafuta mabaki ya ndege iliotoweka laendelea Indonesia

Waokoaji wanakwenda Mashariki mwa Indonesia kutafuta mabaki ya ndege ya abiria iliyokuwa na abiria 54 kutoweka siku ya Jumapili mwishoni mwa juma lililopita.

Timu ya taifa ya utafutaji na uokoaji ya Indonesia, picha ilipigwa Agosti 17 mwaka 2015 katikati ya mji wa Jayapura.
Timu ya taifa ya utafutaji na uokoaji ya Indonesia, picha ilipigwa Agosti 17 mwaka 2015 katikati ya mji wa Jayapura. National Search and Rescue chief Bambang Soelistyo (R) gestures
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii inakuja baada ya kuonekana kwa vipande vya ndege hiyo iliyopoteza mawasiliano ikitokea mjini Jayapura katika mkoa wa Papua.

Ripoti zinasema ndege hiyo ilikuwa na abiria 44 watu wazima na watoto watano na juhudi za kutafuta miili na mabaki ya ndege hiyo zinaendelea.

Inaripotiwa kuwa ndege hiyo ilionekana ikianguka katika Mlima mmoja karibu na eneo la Oksibil.

Kiongozi wa kikosi cha uokoaji Bambang Soelistyo, amesema kuwa moshi ulionekana ukifuka katika eneo hilo.

Hii ndio ajali ya hivi karibuni kutokea barani Asia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.