Pata taarifa kuu
NEPALI-KATIBA-MAANDAMANO-USALAMA

Nepal: maandamano yenye vurugu dhidi ya mswada wa Katiba

Kwa siku ya pili mfululizo nchini Nepal makabiliano kati ya polisi na waandamanaji yalizuka Jumanne wiki hii. Chanzo cha makabiliano hayo, rasimu mpya ya Katiba ambayo inapania kugawanya nchi katika majimbo manane na kusababisha ghadhabu kwa wananchi. Mamia ya watu walijeruhiwa katika maandamano hayo.

Waandamanaji wakikuchoma nakala ya rasimu mswada wa Katiba katika mji wa Kathmandu, Julai 21 mwaka 2015.
Waandamanaji wakikuchoma nakala ya rasimu mswada wa Katiba katika mji wa Kathmandu, Julai 21 mwaka 2015. AFP PHOTO/ Prakash MATHEMA
Matangazo ya kibiashara

Wawakilishi wa Bunge la Katiba walitumwa katika maeneo mbalimbali nchini kukusanya maoni ya raia juu ya rasimu ya Katiba, lakini walipokelewa na vurugu, huku wakirushiwa mawe na wananchi ambao hawaungi mkono rasimu hiyo mpya ya Katiba.

Katika nchi yenye makabila mengi, ambayo inakabiliwa na hofu ya kuvunjika kwa umoja wa kitaifa na nia ya kuona kunadidimia jamii ya wanyonge, imekua vigumu kupata usawa katika suala hili.

Katika nyanda za kusini, kwenye mpaka na India, katika jimbo la Tarai, wawakilishi wa jamii ya watu wachache Madhesi walizuia barabara zote kuu. Waandamanaji walichoma moto nakala za rasimu ya katiba. Waandamanaji hao wanaamini kuwa sheria mpya ya msingi, ambayo bado iko katika maandalizi hawapi na fasi watu kutoka jamii zilizotengwa kama vile wao. Watu hao kutoka jamii ya Madhesi wanalaani ukosefu wa maelezo juu ya mpangilio wa majimbo mapya na wana hofu ya njama za kuhujumu wazo la shirikisho.

Kumeshuhudia pia maandamano na makabiliano na Polisi upande wa chama kinachotetea demokrasia (National Democratic Party), chama cha nne chenye wabunge wengi, ambacho kinanapendelea kuwepo na taifa la watu kutoka jamii ya Hindu. Kwa uchache wajumbe 40 wa chama hicho, ikiwa ni pamoja na kiongozi wake Kamal Thapa, walijeruhiwa.

Wakati huo huo katika mji wa Kathmandu, wanawake walikusanyika mbele ya Bunge wakilaani Katiba, wakisema haina usawa wa kijinsia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.