Pata taarifa kuu
NEPAL-TETEMEKO-USALAMA

Zaidi ya watu 40 wauawa Nepal

Zaidi ya watu 40 wameuawa kutokana na tetemeko  kubwa  la  ardhi  lililotokea  Jumanne wiki hii katika  eneo  la  milimani nchini  Nepal. Tetemeko hilo la ardhi limesababisha maporomoko  ya  ardhi na  majengo  kadhaa kuporomoka.

Kimbunga chenye ukubwa wa kipimo cha Richter 7.4 kimepiga katika mji mkuu wa Nepal Kathmandu.
Kimbunga chenye ukubwa wa kipimo cha Richter 7.4 kimepiga katika mji mkuu wa Nepal Kathmandu. REUTERS/Athit Perawongmetha
Matangazo ya kibiashara

Wakuu nchini Nepal sasa wamethibitisha kuwa idadi ya watu waliokufa kutokana na tetemeko jingine jipya lililotokea nchini humo, imepanda na kufikia zaidi ya watu 40.

Tetemeko  hilo  lililokuwa  na ukubwa wa kipimo cha Richter 7.3 limesababisha hasara kubwa katika wilaya  za kaskazini  mashariki  ya  mji  mkuu Kathmandu na kuleta  hofu  katika  taifa  hilo  ambalo  tayari  liko katika  mshituko  mkubwa  na likijaribu  kurejea  katika  hali  ya kawaida.

Tetemeko hilo kubwa lililosikika hadi nchini India, lilisababisha vifo vya watu watatu huko. Mji wa Namche Bazaar, karibu na mlima Everest umeshuhudia maafa makubwa.

Aprili  25 kulishuhudiwa tetemeko  kubwa  nchini Nepal, ambapo watu 8,150  waliuawa na wengine wengi kuwaacha bila makaazi .

Taarifa zilichelewa  kufika  mji  mkuu  Kathmandu  baada  ya tetemeko  la  leo, lakini  maafisa  na  wafanyakazi  wa  mashirika  ya kutoa  misaada  wamesema  wanatarajia  idadi  ya  vifo  itapanda.

Madhara ya tetemeko hili hayajabainika ila inasemekana kuwa lilitikisa mji mkuu wa India New Delhi, vilevile mji mkuu wa Bangladesh Dhaka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.