Pata taarifa kuu
INDONESIA-Usalama wa Anga

Visanduku vyeusi vya AirAsia vyapatikana

Wapiga mbizi nchini Indonesia wamethibitisha kupatikana kwa visanduku vyeusi vya kurekodi data na sauti vya ndege ya AirAsia ambayo ilianguka katika bahari ya Java.

Mkia wa ndege AirAsia QZ8501 ukiondolewa dani ya bahari JAva na kuwekwa kwenye meliya Indonesia, 10 Januari mwaka 2015
Mkia wa ndege AirAsia QZ8501 ukiondolewa dani ya bahari JAva na kuwekwa kwenye meliya Indonesia, 10 Januari mwaka 2015 REUTERS/Prasetyo Utomo/Pool
Matangazo ya kibiashara

Wataalamu wa kimataifa, hata hivyo, wamesema hawajaweza kuviondoa kutoka chini ya bahari kwa sababu vimekwama kati ya vipande viwili vya ndege hiyo.

Wizara ya uchukuzi ya Indonesia imesema, leo Jumatatu kuwa watalaamu hao wanatarajiwa kukiondoa majini kipande cha ndege hiyo kwa kutumia mifuko maalum ya majini na kuviondoa visanduku hivyo.

Maafisa wanaamini kuwa wahanga wengi wa ajali hiyo bado wamekwama ndani ya kipande cha katikati cha ndege hiyo. Jumapili Januari 11, kipande cha mkia kiliondolewa majini lakini wataalamu hawakupata visanduku hivyo vya kurekodi mawasiliano.

Kufikia sasa miili 48 kati ya watu 162 waliokuwemo ndani ya ndege hiyo imepatikana.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.