Pata taarifa kuu
BANGLADESH-SIASA-SHERIA-USALAMA

Upinzani wanyooshewa kidole Bangladesh

Mamlaka nchini Bangladesh zinatishia kumfungulia mashtaka ya mauaji kiongozi wa chama cha upinzani nchini humo, Khaleda Zia.

Polisi ya Bangladesh ikitoa ulinzi mbele ya nyumba ya Khaleda Zia, kiongozi wa chama kikuu cha upinzani, Januari 4 mwaka 2015.
Polisi ya Bangladesh ikitoa ulinzi mbele ya nyumba ya Khaleda Zia, kiongozi wa chama kikuu cha upinzani, Januari 4 mwaka 2015. AFP PHOTO/ Munir uz ZAMAN
Matangazo ya kibiashara

Polisi wamemkamata naibu wa kiongozi wa chama cha upinzani kwa tuhuma za kuchochea machafuko nchi nzima.

Tishio hili la serikali linatolewa wakati huu ambapo upinzani ukitaka kuchukuliwa kwa hatua dhidi ya polisi waliohusika na mauaji ya wafuasi wake watatu Jumatatu ya wiki hii, na kutaka kufanyika kwa mazungumzo ili kupata suluhu ya kisiasa.

Adilur Rachman Kahn ni katibu mkuu wa chama cha Bangladesh Nationalist amesisitiza kufanyika kwa mazungumzo kuliko nguvu inayotumiwa sasa na serikali.

Upinzani unasisitiza kuwa uchaguzi wa mwaka uliopita haukuwa huru na haki na ulikuwa na kasoro nyingi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.