Pata taarifa kuu
INDONESIA-Usalama wa Anga

Ndege ya AirAsia ilitua juu ya maji kabla ya kuzama

Baadhi ya wataalamu wanadhani kwamba ndege ya shirika la AirAsia la Indonesia, ambayo ipo chini ya bahari Java nchini Indonesia, ilitua kwa dharura juu ya bahari kabla ya kuzama, baada ya kuzidiwa na mawimbi marefu.

Jeshi la anga la Indonesia likiendesha zoezi la kuitafuta ndege ya shirika la AirAsia QZ 8501 tarehe 1 Januari mwa 2015.
Jeshi la anga la Indonesia likiendesha zoezi la kuitafuta ndege ya shirika la AirAsia QZ 8501 tarehe 1 Januari mwa 2015. REUTERS//Dewi Nurcahyani
Matangazo ya kibiashara

Ndege hiyo ya AirAsia, ambayo iliondoka Jumapili Desema 28 mwaka 2014 katika mji wa Indonesia wa Surabaya ikiwa na abiria 162, ilitoweka muda mchache baada ya kukosa mawasiliano na kupaa juu ya bahari ya Java wakati kulipotokea dhoruba. Jambo ambalo si kawaida, marubani hawakuomba msaada wowote, wala hakuna ishara yoyote iliyoonekana wakati ndege hiyo ilipotoweka au kuzama chini ya maji.

Taarifa hii inaelezwa kwamba kwa baadhi ya wataalam kama rubani Iriyanto, rubani wa zamani wa jeshi la anga mwenye taaluma na uzowefu, ambaye alikua akiongoza ndege hiyo, alijaribu kutua kwa usalama, na ndio maana hakuna ishara iliyooneka wakati ilipotoweka. " Uchambuzi wangu ni kwamba ishara haikuonekana kwenye rada kwa sababu hapakua na athari kubwa wakati wa kutua", mhariri wa gazeti linalochapisha taarifa za safari za ndege Angkasa, Dudi Sudibyo, ameliambia shirika la habari la Ufaransa AFP. Kwa mujibu wa Sudibyo, " rubani alijaribu kutua kwenye juu ya maji."

Ndege ya AirAsia ilikua ikuruka kwenye urefu wa mita 9800 wakati rubani alipoomba kugeuza ndege ili kuepuka dhoruba. Ingawa alipewa ruhusa, hakuruhusiwa papo hapo kuruka kwenye urefu uliyo chini ya mita 9800 kutokana na kuepuka kugongana na ndege zingine.

Muda mfupi baadaye ndege hiyo ilipoteza mawasiliano. Baadhi ya wachambuzi wamependekeza kwamba ndege ilifanya ilidondoka kwa sababu ilikuwa ikuruka polepole mno au rubani aliharakia kushuka na kuingoza ndege kwenye urefu wa chini kabisa. Lakini suala la kukosekana kwa ishara kwenye rada limezua utata.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.