Pata taarifa kuu
INDONESIA-ASIA-TSUNAMI-HALI YA HEWA

Miaka kumi baada ya kutokea kwa Tsunami

Miaka kumi imepita tangu bara la Asia likumbwe na kimbunga chenye upepo mkali kiliyojulikana kama Tsunami. Upepo huo ulikua unakwenda kwa kasi kati ya kilomita 500 na 800 kwa saa.

Picha ya marina Madras iliyonaswa na satelaiti nchini India, Desemba 26 mwaka 2014.
Picha ya marina Madras iliyonaswa na satelaiti nchini India, Desemba 26 mwaka 2014. REUTERS/Babu/Files
Matangazo ya kibiashara

Ilikua Desemba 26 mwaka 2004 saa 1 na dakika 58 asubuhi ( saa za Indonesia) wakati kimbunga hicho kilipoanza kuvuma katika bahari Hindi pwani ya Indonesia. Takriban watu 226,000 walifariki katika eneo la Asia ya Kusini.

Kimbunga hicho chenye ukubwa wa Richter 9.1 kilikua ni cha pili chenye nguvu kuwahi kuorodheshwa duniani.

Raia wa Indonesia wameadhimisha leo Ijumaa Desemba 26 miaka 10 tangu kutokea kwa Tsunami. Raia hao wamekusanyika karibu na jengo la makumbusho la tsunami katika eneo la Banda Aceh katika kisiwa cha Sumatra.

Mji huo ulisambaratishwa kabisa na tetemeko kubwa la ardhi na mawimbi ya Tsunami. Makamu wa Rais wa Indonesia, Jusuf Kalla, anatazamiwa kuongoza maadhimisho hayo.

Wafanyakazi wa kujitolea katika eneo hilo na duniani kote walisaidia eneo la Aceh kurejea katika hali ya kawaida baada ya mkasa huo kutokea.

Indonesia iliathirika zaidi kati ya nchi ziliyo kumbwa na kimbunga hicho, ambapo watu 170,000 walifariki kutokana na Tsunami.

Jinsi mawimbi ya bahari hindi na upepo mkali viliyosababisha Tsunami ya mwaka 2004.
Jinsi mawimbi ya bahari hindi na upepo mkali viliyosababisha Tsunami ya mwaka 2004. Creative commons/RobinL

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.