Pata taarifa kuu
CHINA-Maandamano-Siasa

Maandamano Hong Kong: China yatuhumu baadhi ya nchi kuchochea vurugu

Makabiliano mapya kati ya waandamanaji na polisi yametokea Leo Jumapili Oktoba 19 katika mji wa Hong Kong.  

Polisi ikijaribu kuwaondoa waandamanaji katika mji wa kibiashara wa Mangkok, Hong Kong.
Polisi ikijaribu kuwaondoa waandamanaji katika mji wa kibiashara wa Mangkok, Hong Kong. REUTERS/Bobby Yip
Matangazo ya kibiashara

Vurugu hizo zimetokea wakati polisi imekua ikijaribu kuwaondoa wanadamanaji katika mji wa kibiashara wa Mangkok, moja ya maeneo matatu yanayodhibitiwa na waandamanaji kwa muda wa wiki nee sasa.

Hata hivyo vyombo vya habari katika mji wa Hong Kong vimelani nguvu ziliyotumiwa na polisi siku moja iliyopita na kusababisha hali ya sintofahamu katika mji huo. Zaidi ya waandamanaji ishirini walijeruhiwa katika makabiliano hayo. Kwa upande wao viongozi wametuhumu majeshi ya “nje” kuchochoa vurugu hizo.

Viongozi wa Hong Kong wameahidi kukutana kwa mazungumzo na wanafunzi wa vyuo vikuu wanaoandamana Jumaanne Oktoba 21 mwaka 2014.

Kwa mujibu wa afisa mmoja wa serikali, mazungumzo hayo yatarushwa moja kwa moja na yatajikita kwenye mageuzi ya Katiba. Waandamanaji wanadai uwepo wa mfumo wa uchaguzi uliyo huru na wa wazi kwa kuwapigia kura wawakilishi wao, madai ambayo yanapingwa na serikali ya Pekin.

Mkuu wa jimbo la Hon Kong, amesema kupitia mtandandao wa serikali ya Hong Kong kwamba serikali kuu ya China imeelezea wasiwasi wake juu ya kuongezeka kwa vurugu katika mji wa Hong Kong.

“ Serikali kuu ya china imesema ina imani na viongozi wa jimbo la Hong Kong”, amesema mkuu wa jimbo la Hong Kong. Kwa upande wa serikali kuu ya China hata mkuu wa Jimbo la Hong Kong amenyooshea kidole mashirika ya raia wa kigeni kwamba yanashiriki katika maandamano hayo.

“ Mashirika na raia waisiokuwa wakaazi wa Hong Kong wamekua wakichochea vurugu kupitia maandamano yanayoendelea Hong Kong, kama tunavyoshuhudia katika baadhi ya mataifa duniani”, serikali kuu ya china imesema katika tangazo iliyoto Jumapili Oktoba 19 mwaka 2014.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.