Pata taarifa kuu
VIETNAM-Ajali-Usalama

Vietnam : zaidi ya watu 15 wafariki katika ajali ya helikopta ya jeshi

Helikopta ya jeshi la Vietnam imedondoka katika mji wa Hanoi wakati ilipokua katika mazoezi, na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 15 na kujeruhi wengine zaidi ya 5, amesema kiongozi mmoja wa Vietnam, huku vyombo vya habari vya serikali vikitoa idadi ya vifo vya watu zaidi ya 10 nawengine wanane kujeruhiwa.

Jeshi la Vietnam limeanzisha uchunguzi kuhusu chanzo cha ajali ya helikopta ya kijeshi, ailiyoanguka katika mji wa Hanoi.
Jeshi la Vietnam limeanzisha uchunguzi kuhusu chanzo cha ajali ya helikopta ya kijeshi, ailiyoanguka katika mji wa Hanoi. Reuters
Matangazo ya kibiashara

Helikopta hio yenye chapa Mi-171, iliyotengenezwa nchini Urusi imedondoka mapema asubuhi katika wilaya ya Thach That, magharibi mwa mji wa Hanoi, amesema mwanajeshi mmoja ambae hakutaka jina lake litajwe.

“Ndani ya helikopta hio, walikuwemo watu wengi. Tunachunguza eneo na chanzo cha ajali hio”, amesema mwanajeshi huyo, bila hata hivo kutoa taarifa zaidi kuhusu ajali hio, iliyotokea wakati wa mazoezi ya wanajeshi wa anga.

Vyombo vya habari vya serikali vimekua vikitoa taarifa tofauti kuhusu ajali ya helikopta hio. Gazeti la kila siku la Tuoi Tre limechapisha kuwa watu yumkini wanane wamejeruhiwa katika ajali hii, huku kituo cha televisheni cha VTC kikitangaza kuwa zaidi ya watu kumi walifariki katika ajali hii na wengine sita wamejeruhiwa.

Mwaka 2008, marubani watano, ambao ni wanajeshi wa Vietnam walifariki katika ajali ya ndege iliyotengenezwa nchini Urusi, ambayo ilianguka pia katika mji wa Hanoi wakati wa mazoezi ya kijeshi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.