Pata taarifa kuu
PAPUA NEW GUINEA

Watu 200 waokolewa baada ya kivuko kuzama nchini Papua New Guinea

Zaidi ya watu mia mbili wameokolewa katika pwani ya bahari ya nchi ya Papua New Guinea baada ya kivuko walichokuwa wakisafiria kuzama kaskazini mwa nchi hiyo kwenye mpaka wake na Australia.

Waziri mkuu wa Papua New Ginea, Peter O'Neill
Waziri mkuu wa Papua New Ginea, Peter O'Neill Reuters
Matangazo ya kibiashara

Mkuu wa kitengo cha wanamaji nchini humo Nurur Rahman, amedhibitisha kikosi chake kufanikiwa kuwaokoa watu hao mia mbili wakiwa hai na kwamba bado wanaendelea na juhudi za kuwasaka manusura wengine kabla ya jua halijazama.

Kivuko hicho ambacho kinakadiriwa kuwa kilikuwa na abiria zaidi ya 350 kilizama muda mchache baada ya kutoa nanga kwenye bandari ya nchi hiyo ambapo manusura wa ajali hiyo wamesema kuwa kilipata hitilafu kabla ya kuanza kuzama.

Mamlaka nchini humo zimesema kuwa bado zaidi ya watu mia moja na hamsini bado hawajapatikana na kwamba zoezi la uokoaji bado linaendelea ili kujaribu kuona kama kuna watu wengine wanaweza kupatikana wakiwa hai.

Waziri mkuu wa Australia, Julia Gilard amesema kuwa ajali hiyo ni mbaya na kwamba vikosi vya nchi yake kwa kushirikiana na vile vya Papua New Guinea vinaendelea na uokoaji na kwamba nchi yake inafuatilia kuona kama kivuko hicho kilibeba pia raia kutoka nchini Australia.

Waziri mkuu wa Papua New Guinea, Peter O'Neil amesema kuwa polisi wanaendelea na uchunguzi kubaini chanzo cha ajali hiyo na kuongeza kuwa kwasasa hakuna chochote ambacho kimebainika kusababisha ajali hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.