Pata taarifa kuu
Afghanistan

Mashambulizi mawili yaua watu 58 Afghanstan

Mashambulizi mawili katika maeneo tofauti yaliyokuwa yakiwalenga waislam wa kishia yamesababisha watu wasiopunguwa 58 nchi kuuawa.Katika shambulizi lililotokea katika mji wa Kabul watu wapatao 54 wameuawa ambapo mtu anayedhaniwa kuwa alikuwa na bomu la kujitoa mhanga alijichangana na waumini wa kiislam na bomu hilo kulipuka.

REUTERS/ Ina Fassbender
Matangazo ya kibiashara

Shambulio la pili lilitokea karibu na msikiti wa kishia kaskazini mwa Mji wa Mazar-i-Sharif kwa wakati uleule na kusababisha watu wanne kuuawa.

Mashambulizi yamefanyika huku kukiwa na sherehe za mwezi wa Ashura sherehe ambazo ni muhimu sana kwa dhehebu la Shia na zinaadhimishwa kwa mapuziko ya umma.

Mashambulizi ya hayo bado yanaongeza wasiwasi kwa raia wa Afghanstan wakati jitihada za jumuiya kimataifa zikifanyika kuhakikisha kuwa nchi hiyo iko salama.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.