Pata taarifa kuu
MAREKANI-TRUMP-SENETA-SIASA

Trump asherehekea hatua ya kuondolewa mashtaka na Seneti

Rais wa Marekani Donald Trump amekuwa akisherehekea kile anachosema ni ushindi, baada ya Baraza la Seneti kumwondolea mashtaka ya utumiaji mbaya wa madaraka kwa kulidharau bunge yaliyokuwa yanamkabili.

Rais wa Marekani Donald Trump akionesha Gazeti lililoandika habari ya kusafishwa kwake. 06.02.2020
Rais wa Marekani Donald Trump akionesha Gazeti lililoandika habari ya kusafishwa kwake. 06.02.2020 REUTERS/Joshua Roberts
Matangazo ya kibiashara

Trump amesema hakufanya kosa lolote, na kilichokuwa kinaendelea ni vita kutoka kwa maadui wake wa kisiasa, aliowaita mafisadi.

“Nimefanya makosa mengi katika maisha yangu, nakubali....lakini haya ndio matokeo yake,” alisema huku akiinua gazeti lililoandika, “Trump afutiwa mashtaka”.

“Tulipitia wakati mgumu sana, tuliteseka. Hatukufanya kosa lolote,” aliongeza rais Trump.

Licha ya kusafishwa na baraza la Seneti, Trump alipigiwa kura ya kukosa imani naye na bunge la wawakilishi mwezi Desemba mwaka 2019 kwa makosa ya matumizi mabaya ya madaraka na kulidharau bunge.

Macho sasa yanaelekezwa katika kampeni za kuelekea Uchaguzi Mkuu mwezi Novemba ambao sasa utaamua hatima ya rais Trump ambaye anatarajiwa kukubaliwa na upinzani mkubwa kutoka kwa wagombea wa chama cha Democratic.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.